Breaking News

Aya 113 – 122: Tumeitermsha Qur’an Kwa Lugha Ya Kiarabu

Aya 113 – 122: Tumeitermsha Qur’an Kwa Lugha Ya Kiarabu

Maana

NamnhiytumeiteremshQur’akwlughykiarabna tumekariri humo maonyo ili wawe na takua auiwaletee makumbusho.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameteremsha Qur’an kwa mja wake Muhammad (s.a.w.) kwa lugha ya kiarabu na akawahadharisha waja na hisabu yake na adhabu yake, kwa mifumo mbalimbali, ili wapate kumcha na kumtii kwenye hukumu zake zote au awamkumbuke yeye wanapofanya madhambi ili watubu na wamwombe msamaha. Au hapa, ni kwa maana ya na; kama mfano ukisema: “Kuwa mwana wa chuoni au mwenye zuhudi.” Kwa sababu kukumbuka kuko pamoja na takua; kama ambavyo zuhudi iko pamoja na elimu.
Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 12 (12:2). Huko tumejibu kwa ufafanuzi swali la mwenye kuuliza, kwa nini Qur’an imeteremshwa kwa lugha ya kiarabu pamoja na kuwa Muhammad (s.a.w.) ametumwa kwa watu wote?

Wasifu Wa Qur’an

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameitaja Qur’an, katika kitabu chake kitukufu, kwa sifa nyingi, zikiwemo hizi zifuatazo:
1. Ya kiarabu; kama ilivyo katika Aya hii na ile ya Juz. 12 (12:2).
2. Ukumbusho:
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ {9}
“Na hakika sisi tumeuteremsha ukumbusho huu.” Juz. 14: (15:9).
3. Nuru:
قَدْ جَاءَكُمْ مِنَ اللَّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُبِينٌ {15}
“Hakika imekwishawafikia nuru kutoka kwa MwenyeziMungu” Juz. 6: (5:15).
4. Upambanuzi:
إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ {13}
“Hakika hiyo ni kauli ya upambanuzi” (86:13).
5. Uongofu: “Hicho ni kitabu, hakina shaka ndani yake, ni uongofu kwa wenye takua.” Juz. 1 (2:2).
6. Hekima:
وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ {2}
“Naapa kwa Qur’an yenye hekima” (36:2).
7. Roho: “Naapa kwa Qur’an Tukufu” (50:1).
8.
رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنْذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ {15}
“Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katikawaja wake, ili kuonya kwa siku ya makutano” (40:15).
9. Haki:
إِنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ {17}
“Hakika hiyo ni haki itokayo kwa Mola wako. Lakini watu wengi hawaamini.”Juz. 12 (11:17).
10. Habari kubwa: “Sema: Hiyo ni habari kubwa ambayo nyinyi mnaipuuza.” (38:67–68).
11. Ponyo:
قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ {44}
 Sema: hiyo ni uongofu na ponyo kwa wenye kuamini”(41:44).
12. Rehema:
وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ {77}
“Na hakika hiyo ni uwongofu na rehema kwa waumini”(27:77).
13. Uteremsho:
تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ {80}
“Ni uteremsho utokao kwa Mola wa walimwengu wote”(56:80).
14. Bishara na onyo:
كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ {3}
بَشِيرًا وَنَذِيرًا {4}
“Ni Kitabu kilichopambanuliwa Aya zake, cha kusomwakwa kiarabu kwa watu wanaojua, kinachotoa bishara nakuonya” (41:3  4).
15. Nguvu na utukufu:
وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ {41}
“Na hakika ni Kitabu chenye nguvu na utukufu.” (41:41).
16. Adhimu:
وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ {87}
“Na hakika tumekupa Aya saba zinazorudiwa rudiwa naQur’an Adhimu.” Juz. 14 (15:87).
17. Ubainifu:
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ {2}
“Naapa kwa Kitabu kinachobainisha” (43:2).
Hakika bora zaidi inayofahamisha sifa hizi ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameteremsha Qur’an kwa Mtume wake, kwa ajili tu ya kuwaongoza watu kwenye wema, amani na utulivu wao.
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa haki.
Imam Ali (a.s.) anasema, akilingania Mola wake: “Kutakata ni kwako! Ni utukufu ulioje wa tunayoyaona katika uumbaji wako! Na udogo ulioje wa hayo katika uweza wako! Na ni vituko vilioje wa tuvionavyo katika ufalme wako! Na ni uduni ulioje wa tusivyoviona katika ufalme wako! Na ueneaji ulioje wa neema zako katika dunia! Na ni udogo ulioje wa neema hizo kulinganisha na neema za Akhera!”
Wala usiifanyie haraka hii Qur’an kabla haujamalizikawahyi wake
Kuna Hadith isemayo kuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa anapoletewa Qur’an na Jibril hufuatilia kuisoma kwa kuhofia kisimpite kitu, ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha asikilize tu wala asifuatishe na kwamba atulie tu wala asiogope kusahau. Usahihi wa Hadith hii unafahamishwa na ile Aya isemayo:
“Usiutikisie, huu wahyi, ulimi wako kwa kuufanyia haraka. Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha, kisha ni juu yetu kuubainisha” (75: 16 – 19).

Nizidishe Elimu

Na sema: Mola wangu! Nizidishie elimu
Elimu aliyomwamrisha Mwenyezi Mungu Mtume wake, kuomba kuzidishiwa ni ile inayomnufaisha mwenye nayo na mwenginewe. Hakuna itikadi wala misimamo, falsafa wala sharia au fasihi na sanaa, zote hizi si lolote mbele ya Mwenyezi Mungu ispokuwa kama zitakuwa ni nyenzo za maisha bora yasiyokuwa na matatizo wala vikwazo vyovyote.
Hata maisha ya Akhera yanafungamana moja kwa moja na kazi itakayon- ufaisha katika maisha ya duniani. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema: “Mbora zaidi wa watu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayewafaa zaidi watu.” Hakuna mwenye shaka kwamba anayewafaa zaidi watu ni yule anayefanya kwa ajili ya maisha bora na jamii.
Kila kitu, wakati huu, kinafahamisha waziwazi kuwa hakuna maisha bora ispokuwa kwa elimu; bila ya kutofautisha baina ya maisha ya kimaada, kijamii na kiutamaduni.
Kama ambavyo jamii yoyote haiwezi kuishi maisha bora bila ya mitambo ya kuchapisha, viwanda vya nguo, nyenzo za mawasiliano, vifaa vya nyumbani na maengineyo ya lazima; basi vile vile haiwezekani kuishi huru na heshima bila ya elimu ya siasa, uchumi, ya kijamii na elimu nyinginezo zinazofanya kazi ya kumtumikia mtu kwa ajili ya utu.
Hii ndiyo elimu sahihi na ndiyo iliyokusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na sema: Mola wangu! Nizidishie elimu’ na kauli ya Mtume: “Mwenye kufuata njia ya kutafuta elimu, amefuata njia ya kwenda peponi.”
Yeyote mwenye kufasiri neno elimu kwa maana ya kuhifadhi maandishi na maelezo, basi huyo ni katika wale wanaoamini kuwa elimu ni matamshi na maandishi tu; na dini ni kupiga takbira na kusoma tasbih tu.
Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau walahatukuona kwake azma.
Maagano Alioagana Mwenyezi Mungu na Adam ni kutoukurubuia mti na kwamba asisikilize mwito wa Iblis. Makusudio ya kusahau ni kuacha na azma ni uthabiti.
Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam!Wakasujudu wote ispokuwa Iblisi alikataa.
Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 1 (2:34), Juz. 8 (7:11), Juz. 14 (15: 30 – 31), na katika Juz. 15 ( 17: 61) na (18:50).
Tukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui yako na wamkeo. Basi asiwatoe katika Bustani (Pepo) hii, mkaingia mashakani. Hakika humo hutakuwa na njaa walahutakuwa uchi. Na kwamba wewe hutapata kiu humowala hutapata joto.
Yaani hutatabika kwenye joto la jua. Neno joto tumelifasiri kutoka neno Dhuha lenye maana ya mchana. Umetumika mchana kwa maana ya joto kwa vile mchana kunakuwa na joto kali.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimuhadharisha Adam kutokana na wasiwasi wa Ibilisi na akamwambia, wewe una hiyari ya mambo mawili; ama unitii mimi na umuasi Ibilisi upate hii Pepo (Bustani) – kama uinavyo – safi na nzuri. Humo hamna njaa, kiu, kukaa uchi wala maradhi. Hamna maumivu wala huzuni, hamna mauti, damu wala machozi, hamna kuhangaika kwenye joto wala baridi. Hamna chochote ispokuwa amani, utulivu na raha.
Au uniasi mimi na kumtii Ibilisi, utoke Peponi uende duniani kwenye taabu, balaa zote, magonjwa na majanga.
Lakini Adam alisahau hadhari hizi; akaandamwa na misukosuko yeye na kizazi chake, kuanzia na kuuliwa Habil hadi uhalifu wa Israil na mengineyo yasiyokuwa na kikomo.
Sio mbali kuwa kutolewa Adam Peponi ni somo na fundisho kwa yule anayefuata matamanio na kwamba malipo yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni adhabu. Angalia kifungu ‘Mtaka yote hukosa yote’ Juz. 1 (2: 35–39).
Lakini shetani alimtia wasiwasi, akamwambia: EwAdam! Nikujulishe mti wa kuishi milele na ufalme usiokoma? Basi wakaula wote na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani yaBustani.
Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 8 (7:19 – 22).
Na Adam akamuasi Mola wake na akapotea njia.
Unaweza kuuliza: Adam ni nabii na nabii ni maasumu wa makosa, imekuwaje Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kumnasibishia uasi na upotevu?
Wamelijibu hilo kwa majibu kadhaa; miongoni mwayo ni kuwa makusudio ya kuasi ni kuacha mapendekezo sio wajibu, jambo ambalo halipingani na isma.
Jibu jingine ni kuwa Adam alipokuwa Peponi alikuwa Akhera ambako hakuna tabligh wala taklifa yoyote ya kuhitajia mitume, na kwamba utume wa Adam ulikuwa wa duniani sio wa Akhera.
Kwa hali yoyote iwayo ni kwamba Adam alitubia na akamuomba msamaha Mola wake; kisha Mola wake akamteua na akamkubalia toba yake na akamwongoa.
Tumeuazungumzia hayo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 1 (2:35–39) kifungu cha ‘isma ya mitume.’
قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ {123}
Akasema: Ondokeni humu nyote; hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukiwafikia uongofu kutoka kwangu, basi atakayefuata uongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ {124}
Na atakayejiepusha na mawaidha yangu, basi hakika atapata maisha yenye dhiki. Na tutamfufua siku yKiyamhalykuwa kipofu.
قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنْتُ بَصِيرًا {125}
Aseme: Ewe Mola wangu! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?
قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنْسَىٰ {126}
Atasema (Allah): Ndivyo hivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahahu na kadhalika leo unasahauliwa.
وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي مَنْ أَسْرَفَ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِآيَاتِ رَبِّهِ ۚ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبْقَىٰ {127}
Na hivyo ndivyo tutakavy- omlipa kila apitaye kiasi na asiyeamini ishara za Mola wake. Na Hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi na inadumu.
أَفَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِأُولِي النُّهَىٰ {128}
Je, haikuwabainikia, ni vizazi vingapi tuliviangamiza kabla yao nao wanatembea katika maskani zao. Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kwa wenye akili.
وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِنْ رَبِّكَ لَكَانَ لِزَامًا وَأَجَلٌ مُسَمًّى {129}
Na lau si neno la Mola wako lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako na muda uliotajwa, bila shaka ingelikuwalazima.


Hakuna maoni